Sinopse

Nyumba ya Sanaa ni Makala ya  Utamaduni ambayo inatoa fursa  kwa wasanii  na wadau wa sanaa kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Afrika na dunia kwa ujumla, tukiwa na lengo la kudumisha na kuendeleza tamaduni nzuri katika mwingiliano wa tamaduni uliopo, tukizingatia maisha ya kisasa na utandawazi kwa ujumla.

Episódios

 • Nyumba ya Sanaa - Ushairi umesaidia kukuza Fasihi

  Nyumba ya Sanaa - Ushairi umesaidia kukuza Fasihi

  14/12/2019 Duração: 20min

  Umuhimu wa Ushairi katika kukuza fasihi,Kutana na Steven Mumbi katika Mkala ya Nyumba ya sanaa.

 • Nyumba ya Sanaa - Maudhui katika sanaa ya filamu nchini Kenya

  Nyumba ya Sanaa - Maudhui katika sanaa ya filamu nchini Kenya

  16/11/2019 Duração: 20min

  Serikali ya Kenya imeendelea kutilia mkazo suala la kukagua maudhui ya kazi za sanaa nchini humo kwa lengo la kuhakikisha kuwa, ujumbe wa filamu na muziki sio wa kupotosha. Tunaangazia hili na afisa katka bodi ya filamu nchini humo Bonventure Kioko.

 • Nyumba ya Sanaa - Wamwiduka wakifanya Onesho Mtaani

  Nyumba ya Sanaa - Wamwiduka wakifanya Onesho Mtaani

  12/11/2019 Duração: 20min

  Bendi ya Muziki inayofanya Sanaa ya Muziki kwa kupiga mtaa kwa Mtaa wazungumzia namna walivyofanikiwa kuifanya sanaa hiyo kutokea mkoani Mbeya Nyanda za juu kusini mwa Tanzania mpaka jijini Dar es salaam kufanya sanaa hii. Ungana na Steven Mumbi katika Makala haya akizungumza na Viongozi wa Bendi hiyo.

 • Nyumba ya Sanaa - Koshuma Sanaa ya Urembo inalipa zaidi ya Kuajiriwa

  Nyumba ya Sanaa - Koshuma; Sanaa ya Urembo inalipa zaidi ya Kuajiriwa

  31/10/2019 Duração: 20min

  Sanaa ya Urembo ni Sanaa nyingine inayokuwa kwa kasi miongoni mwa Vijana, Wasichana wanatumia fursa ya kuwaremba si Maharusi tu hivi sasa hata watu wa kawaida wanapenda kurembwa katika sura zao ili kuonekana warembo na Watanashati katika shughuli zao za Kawaida. Makala haya yameangazia Sanaa hii, Steven Mumbi amezungumza na Hilda Koshuma, Mwalimu na Msanii anayefanya Sanaa hii

 • Nyumba ya Sanaa - Ngumba Uchoraji wa Picha Halisi unavutia Watalii

  Nyumba ya Sanaa - Ngumba; Uchoraji wa Picha Halisi unavutia Watalii

  14/10/2019 Duração: 20min

  Sanaa ya Uchoraji wa picha Halisi ni Sanaa nyingine inayopendwa nchini Tanzania, kutana na Mchoraji Agasto Ngumba akizungumzia Sanaa hiyo katiak Makala haya.

 • Nyumba ya Sanaa - Wadatoga na Wamasai wanajivunia Sanaa ya Uimbaji nchini Tanzania

  Nyumba ya Sanaa - Wadatoga na Wamasai wanajivunia Sanaa ya Uimbaji nchini Tanzania

  14/10/2019 Duração: 20min

  Wadatooga (pia huitwa Wataturu au Wamang'ati) ni kabila la watu wa Kiniloti nchini Tanzania wanaoishi hasa katika mikoa ya Manyara, Mara, Arusha na Singida. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na kikundi cha WADACA kutoka Ngorongoro kaskazini mwa Tanzania.

 • Nyumba ya Sanaa - Kutana na Mchoraji wa Vibonzo Muhidin Msamba

  Nyumba ya Sanaa - Kutana na Mchoraji wa Vibonzo 'Muhidin Msamba'

  26/08/2019 Duração: 20min

  Ungana na Steven Mumbi akizungumza na Mchoraji wa Vibonzo Muhidini Msamba kuhusu safari yake ya sanaa na Mapokeo ya sanaa hiyo kwa Ujumla.

 • Nyumba ya Sanaa - Malkia Queens Wasichana Wasanii wanaojivunia kuwa Wachoraji

  Nyumba ya Sanaa - Malkia Queens; Wasichana Wasanii wanaojivunia kuwa Wachoraji

  11/06/2019 Duração: 20min

  Upatikanaji wa Vifaa,Gharama pamoja na Uelewa Duni vinachangia Sanaa ya Uchoraji kushindwa kusonga Mbele. Malkia Queens wazungumza na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.

 • Nyumba ya Sanaa - MonalisaKazi za Sanaa za Wanawake hazijanadiwa vya kutosha

  Nyumba ya Sanaa - Monalisa;Kazi za Sanaa za Wanawake hazijanadiwa vya kutosha

  11/06/2019 Duração: 20min

  Makala ya Nyumba ya Sanaa inaangazia changamoto wanazokabiliana nazo wanawake Waigizaji kiasi cha kuwalazimisha kugeukia kazi nyingine ili kujipatia kipato. Ungana na Steven Mumbi akizungumza na Wasanii mbalimbali nchini Tanzania.

 • Nyumba ya Sanaa - Wawanawake waaswa kujitokeza kufanya Sanaa za Mikono

  Nyumba ya Sanaa - Wawanawake waaswa kujitokeza kufanya Sanaa za Mikono

  11/06/2019 Duração: 19min

  Nyumba ya Sanaa inaangazia Sanaa ya Ususi ama Ufumaji kutoka Mkoani Morogoro Nchini Tanzania. Mtangazaji wa Makala haya Steven Mumbi anazungumza na Kiongozi wa Kikundi cha Mkonge Sisal.

 • Nyumba ya Sanaa - Hali ya Muziki na Wanamuziki wa Tanzania

  Nyumba ya Sanaa - Hali ya Muziki na Wanamuziki wa Tanzania

  16/05/2019 Duração: 19min

  Kutana na Imelda Munyaga Mwalimu wa Sanaa za aina mbalimbali. Katika Makala haya anazungumza na Steven Mumbi kuhusu Sanaa ya Muziki na Uigizaji.

 • Nyumba ya Sanaa - Waimbaji wa Muziki wa Injili Wabadilike

  Nyumba ya Sanaa - 'Waimbaji wa Muziki wa Injili Wabadilike'

  29/04/2019 Duração: 20min

  Allain Nyangasa awataka Waimbaji wa Muziki wa Injili kubadilika kufanya Muziki wa Injili kwa ajili ya kumtumikia Mungu na si Biashara Ungana na Steven Mumbi katika Makala haya akizungumza na Msanii huyo.

 • Nyumba ya Sanaa - MlokaUshairi wa zamani ulikuwa unakonga nyoyo za Wengi

  Nyumba ya Sanaa - Mloka;Ushairi wa zamani ulikuwa unakonga nyoyo za Wengi

  09/04/2019 Duração: 19min

  Ushairi ni Sanaa iliyotumika kukuza Lugha ya Kiswahili katika Nchi za Afrika Mashariki,ikiwemo Tanzania hasa wakati wa kupigania uhuru na hata baada ya Uhuru katika kuhamasisha watu kufanya Maendeleo. Steven Mumbi amezungumza na Mshairi wa siku nyingi nchini Tanzania,Charles Mloka, Ungana nae katika Makala haya ya Nyumba ya Sanaa.

 • Nyumba ya Sanaa - S.KideMuziki wa Singeli Utafika mbali kama wawekezaji watajitokeza

  Nyumba ya Sanaa - S.Kide;Muziki wa Singeli Utafika mbali kama wawekezaji watajitokeza

  09/04/2019 Duração: 20min

  Muziki wa Singeli ni Miongoni mwa Muziki unaochipukia nchini Tanzania,vijana wanajaribu kuifikia hadhira kwa kutumia maudhui ya Asili. Katika Makala haya ya Nyumba ya Sanaa,Ungana na Steven Mumbi akizungumzia Muziki huo akiwa na S.Kide pamoja na Kiongozi wa Wakupeti Band.

 • Nyumba ya Sanaa - MaidaSanaa ya Ubunifu wa Mavazi imeniwezesha kuwa Mbunifu wa Majengo

  Nyumba ya Sanaa - Maida;Sanaa ya Ubunifu wa Mavazi imeniwezesha kuwa Mbunifu wa Majengo

  26/03/2019 Duração: 19min

  Maida waziri Mwanamke aliyeamua kufanya kazi ya Sanaa na hatimaye kufanikiwa kuwa Mbunifu wa Majengo. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Maidfa Waziri kuhusu safari yake katika Sanaa ya Ubunifu

 • Nyumba ya Sanaa - Usambazaji wa Filamu wawa kikwazo cha Sanaa ya Uigizaji Kuendelea Tanzania

  Nyumba ya Sanaa - Usambazaji wa Filamu wawa kikwazo cha Sanaa ya Uigizaji Kuendelea Tanzania

  19/03/2019 Duração: 20min

   Filamu za Kiswahili ni Miongoni mwa Filamu zinazopendwa sana katika nchi za Afrika Mashariki si kutokana na kuwa zinatumia lugha adhimu ya Kiswahili tu bali pia ni kutokana na Maudhui na upekee zilionao. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akiangazia Sanaa hii na changamoto zinazowakabili Waigizaji nchini Tanzania

 • Cocodo Vijana tujitume zaidi kwenye Muziki

  Cocodo; Vijana tujitume zaidi kwenye Muziki

  09/03/2019 Duração: 20h03min

  Hii ni Sehemu ya Pili ya Makala haya tukiangazia Muziki na Cocodo African Music Band wakifanya sanaa ya Muziki kutoka nchini Tanzania Ungana na Steven Mumbi akizungumza na wasanii Remi na Nelius wakizungumzia safari yao ya kimuziki kwa zaidi ya miaka nane sasa

 • Cocodo Vijana Hawajawekeza kufanya Muziki wa Asili kikamilifu

  Cocodo; Vijana Hawajawekeza kufanya Muziki wa Asili kikamilifu

  02/03/2019 Duração: 20h02min

  Katika Makala haya Tunaangazia Muziki na Cocodo African Music Band wakifanya sanaa ya Muziki kutoka nchini Tanzania Ungana na Steven Mumbi akizungumza na Lemi na Nelius wakizungumzia Safari yao ya kimuziki katika Sehemu hii ya kwanza.

 • Mubanga Watunzi wa Vitabu Wafuate hatua za Utunzi

  Mubanga; Watunzi wa Vitabu Wafuate hatua za Utunzi

  23/02/2019 Duração: 19min

  Teknolojia ina athari gani katika Utunzi wa Vitabu? Ungana na Steven Mumbi akizungumza na Clement Mubanga Mtunzi wa vitabu katika Makala ya Nyumba ya sanaa.

 • Kimbokota Sanaa ya Ubunifu haijawekezwa ipasavyo Mashuleni

  Kimbokota; Sanaa ya Ubunifu haijawekezwa ipasavyo Mashuleni

  16/02/2019 Duração: 19min

  Sanaa ya Ubinufu ndio sanaa mama katika Uchoraji,Uchongaji na hata katika matumizi ya vyuma chakavu katika kuunda Vifaa mbalimbali. Katika Makala ya Nyumba ya Sanaa Ungana na Steven Mumbi akizungumzuza na Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es salaam UDSM, Safina Kimbokota wakizungumza Sanaa hiyo na Mapokeo ya wanafunzi kusoma Sanaa katika elimu ya juu.

Informações: