Sinopse

Huu ni wasaa wa kukutana na wageni mbalimbali watakaokuwa wakifika katika studio zetu na kuzungumza moja kwa moja yaani LIVE. Ni mjadala wa kila Jumatano asubuhi ambao utagusa masuala muhimu yanayoibuka ndani na nje ya Bara la Afrika katika nyanja tofaut itofauti. Mjadala wa wiki ni wasaa utakaokuzungusha dunia nzima kupitia mawimbi ya RFI Kiswahili.

Episódios

 • Mjadala wa Wiki - Miaka minne ya rais wa Tanzania John Magufuli

  Mjadala wa Wiki - Miaka minne ya rais wa Tanzania John Magufuli

  06/11/2019 Duração: 15min

  Rais wa Tanzania John Magufuli, ametimiza miaka minne madarakani, je ni mafaniko gani na changamoto zipi zilizoshuhudiwa kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 ?

 • Mjadala wa Wiki - Hatima ya Uchaguzi Mkuu nchini Msumbiji

  Mjadala wa Wiki - Hatima ya Uchaguzi Mkuu nchini Msumbiji

  16/10/2019 Duração: 12min

  Wananchi wa Msumbiji, wanasubiri matokeo ya Uchaguzi Mkuu baada ya kupiga kura siku ya Jumanne. Ni uchaguzi ambao wachambuzi wa siasa wanasema ni kipimo cha demokrasia na utekelezwaji wa mkataba wa amani uliotiwa saini kati ya waasi wa Renamo na serikali, miezi miwili iliyopita. Tunajadili suala hili.

 • Mjadala wa Wiki - Dunia kuangazia mabadiliko ya tabia nchi

  Mjadala wa Wiki - Dunia kuangazia mabadiliko ya tabia nchi

  25/09/2019 Duração: 11min
 • Mjadala wa Wiki - Rais wa DRC Felix Tshisekedi azuru Ubelgiji kuimarisha uhusiano

  Mjadala wa Wiki - Rais wa DRC Felix Tshisekedi azuru Ubelgiji kuimarisha uhusiano

  18/09/2019 Duração: 13min

  Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi,yupo ziarani nchini Ubelgiji. Ni ziara yake ya kwanza barani Ulaya, baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa DRC mapema mwaka huu. Tshisekedi yupo nchini Ubelgji, kuhimiza ushirikano kati ya nchi hizo mbili, uhusiano ambao ulikuwa baridi wakati wa uongozi wa rais wa zamani Joseph Kabila. Je, ziara hii ina umuhimu gani kwa raia wa DRC na kwanini inazua maswalimengi maswali miongoni mwa raia wa DRC wauishio nje na ndnai ya nchi ?  Kujadiki hili, tunauganba na Raphae Bakema, mchambuzi wa siasa za DRC naeneo la Maziwa Makuu, akiwa Goma lakini Profesa Malonga Pacique akiwajijini Kgali. 

 • Mjadala wa Wiki - Baraza huru laundwa nchini Sudan

  Mjadala wa Wiki - Baraza huru laundwa nchini Sudan

  21/08/2019 Duração: 15min

  Baraza huru kati ya viongozi wa kijeshi na kiraia limeundwa nchini Sudan, kuongoza nchi hiyo kwa muda wa miaka mitatu, je, litatimiza mahitaji ya raia wa Sudan ? Tunajadili.

 • Mjadala wa Wiki - Mkutano wa 39 SADC kuangazia uchumi wa viwanda

  Mjadala wa Wiki - Mkutano wa 39 SADC kuangazia uchumi wa viwanda

  07/08/2019 Duração: 15min

  Karibu katika makala ya mjadala wa wiki.Kikao cha 39 cha viongozi wa mataifa ya SADC kinataraji kuanza jijini Dar es salaam nchini Tanzania ajenda kuu ni kujadili mkakati wa kiuchumi kwa kuhimiza viwanda katika mataifa hayo.Fuatilia kwa kina,wachambuzi Wetengere Kitojo na Saidi Msonga wameangazia kinaga ubaga katika makala haya na mwandishi wetu Martha Saranga.

 • Mjadala wa Wiki - Nani atamaliza Ebola nchini DRC ?

  Mjadala wa Wiki - Nani atamaliza Ebola nchini DRC ?

  24/07/2019 Duração: 15min

  Wiki hii Waziri wa afya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Oly Ilunga alitangaza kujiuzulu, baada ya kushtumu uamuzi wa rais Felix Tshekedi kumwondoa kwenye Kamati maalum ya kupambana na janga la ugonjwa hatari wa Ebola, ambao tangu mwezi Agosti mwaka 2018, umesababisha vifio vya watu 1,700 na wengine zaidi ya 200 kuambukizwa katika jimbo la Kivu Kaskazini. Nani atasaidia kumaliza Ebola nchini DRC na juhudi za WHO zinafua dafu ?

 • Mjadala wa Wiki - Mauaji nchini Ethiopia yanalenga kuharibu mipango ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed ?

  Mjadala wa Wiki - Mauaji nchini Ethiopia yanalenga kuharibu mipango ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed ?

  26/06/2019 Duração: 12min

  Mnadhimu Mkuu wa jeshi  nchini Ethiopia Jenerali Seare Mekonnen ameuawa kwa kupigwa risasi na mlinzi wake jijini Addis Ababa, sawa na rais wa jimbo la Amharic Ambachew Mekonen ambaye alishambuliwa na watu wenye silaha. Ni mauaji yanayokuja wakati huu, Waziri Mkuu Abiy Ahmed akiendeleza mageuzi nchini mwake.     Hii inamaanisha nini ? Tunachambua na wachambuzi wa siasa za Kimataifa Haji Kaburu, Comrad Sambala wote wakiwa jijini Dar es salaam nchini Tanzania. Emmanuel Makundi, anashiriki pia, ni Mwanhabari wa RFI Kiswahili.

 • Mjadala wa Wiki - Machafuko nchini Sudan, maafa na majeruhi yaripotiwa

  Mjadala wa Wiki - Machafuko nchini Sudan, maafa na majeruhi yaripotiwa

  05/06/2019 Duração: 14min

  Wiki hii, uongozi wa kijeshi nchini Sudan, uliamua kuvunja kambi ya waandamanaji jijini Khartoum ambao wamekuwa wakishinikiza jeshi kukabidhi madaraka kwa raia.Watu zaidi ya 60 walipoteza maisha na mamia kujeruhiwa. Nini hatima ya Sudan ? Tunajadili.

 • Mjadala wa Wiki - DRC yampata Waziri Mkuu baada ya kusubiri miezi mitano

  Mjadala wa Wiki - DRC yampata Waziri Mkuu baada ya kusubiri miezi mitano

  23/05/2019 Duração: 12min

  Hatimaye rais wa DRC Felix Tshisekedi amemteua Sylvestre Ilunga kuwa Waziri Mkuu. Hii inakuja baada ya mashauriano ya muda mrefu kati ya rais huyo na mwenzake wa zamani Joseph Kabila. Matarajio ya raia wa DRC ni nini ?

 • Mjadala wa Wiki - Kiongozi wa upinzani nchini DRC Martin Fayulu ataka maandamano dhidi ya rais Tshisekedi

  Mjadala wa Wiki - Kiongozi wa upinzani nchini DRC Martin Fayulu ataka maandamano dhidi ya rais Tshisekedi

  02/05/2019 Duração: 15min

  Kiongozi wa upinzani nchini DRC Martin Fayulu, anataka maandamano yafanyike nchini humo kumshinikiza rais Felix Thisekedi aondoke madarakani kama ilivyokuwa nchini Sudan na Algeria. Fayulu anasema yeye ndiye aliyeshinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2018. Tunachambua hili kwa kina.

 • Mjadala wa Wiki - Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika ajiuzulu

  Mjadala wa Wiki - Rais wa Algeria Abdelaziz Bouteflika ajiuzulu

  03/04/2019 Duração: 12min

  Baada ya kuwa madarakani kwa miaka 20 hatimaye Abdulaziz Bouteflika amelazimika kusalimu amri na kujiuzulu kama rais wa nchi wa Algeria. Nini hatima ya nchi ya Algeria baada ya kujiuzulu kwa Bouteflika mwenye umri wa miaka 82 ambaye tangu mwaka 2013 amekuwa akitumia gari la magurumu baada ya kupatwa na kiharusi. Kwa mujibu wa Katiba, Spika wa Senate sasa ndio rais wa muda hadi pale Uchaguzi mpya utakapofanyika.

 • Mjadala wa Wiki - IS ladhoofishwa Syria na Iraq

  Mjadala wa Wiki - IS ladhoofishwa Syria na Iraq

  27/03/2019 Duração: 12min

  Baada ya miezi ya mapigano, kikundi cha jihadi cha Kiislam (IS) kimepoteza Baghuz, kijiji cha mashariki mwa Siria ambacho kinaelezwa kuhitimisha utawala wa kihalifa nchini syria.Kama ambavyo mwishoni mwa 2017, IS ilivyopoteza ngome zake za Mosul nchini Iraq na Raqqa nchini Syria.

 • Mjadala wa Wiki - Mvutano kati ya Rwanda na Uganda Marekani yatia neno

  Mjadala wa Wiki - Mvutano kati ya Rwanda na Uganda Marekani yatia neno

  13/03/2019 Duração: 12min

  Makala ya mjadala inaangazia mvutano wa kidiplomasi akati yamataifa mawili ya Afrika mashariki,Uganda na Rwanda wakati huu jumuiya ya Afrika mashariki ikiwa  kimya..wachambuzi Abbas Mwalimu na Haji Kaburu wanadadavua kwa kina.

 • Mzozo kati ya Rwanda na Uganda kuhusu mpaka wa Katuna

  Mzozo kati ya Rwanda na Uganda kuhusu mpaka wa Katuna

  06/03/2019 Duração: 11min

  Nchi za Rwanda na Uganda zinashuhudia mvutano wa kidiplomasia. Rwanda inaishutumu Uganda kwa kuwaficha maadui wa serikali yake, suala ambalo Uganda inakanusha vikali.

 • Mzozo wa kisiasa nchini Venezuela

  Mzozo wa kisiasa nchini Venezuela

  30/01/2019 Duração: 11min

  Venezuela imejikuta katika mzozo wa kisiasa na kiuchumi, kiongozi wa upinzani  Juan Guaido amejiapisha kuwa rais, huku kiongozi wa nchi hiyo Nicolas Maduro akitishia kumchukulia hatua kali. Tunajadili hili kwa kina.

 • Mustakabali wa DRC baada ya matokeo ya uchaguzi

  Mustakabali wa DRC baada ya matokeo ya uchaguzi

  16/01/2019 Duração: 11min

  Baada ya tume ya uchaguzi nchini DRC CENI kumtangaza mshindi wa kiti cha uraisi mgombea wa upinzani Felix Tshisekedi,tunaangazia nini matarajio ya raia sasa,nini mustakabali wa DRC wakati huu upinzani wa lamuka ukipinga matokeo hayo kwa kudai udanganyifu ulifanyika.

 • Wananchi wa DRC bado wanasubiri matokeo ya Uchaguzi Mkuu

  Wananchi wa DRC bado wanasubiri matokeo ya Uchaguzi Mkuu

  09/01/2019 Duração: 17h01min

  Mamilioni ya raia wa DRC, pamoja na dunia, inasubiri Tume ya Uchaguzi kumtangaza mshindi wa Uchaguzi wa urais, baada ya wananchi kupiga kura Desemba 30 2018. Nani atashinda Uchaguzi huu na ni kwanini matokeo yamechelewa ? Tunachambua suala hili kwa kina.

 • Raia wa DRC waendelea kusubiri matokeo,mtandao wazimwa

  Raia wa DRC waendelea kusubiri matokeo,mtandao wazimwa

  02/01/2019 Duração: 11min

  Makala ya mjadala wa wiki inaangazia hali ya mambo nchini DRC wakati huu raia wakisubiri matokeo ya kura ya uraisi wabunge na viongozi wa wilaya kote nchini humo kunashuhudiwa mtandao ukizimwa kwa sababu kiusalama kama ambavyo serikali imeeleza...karibu,wazungumzaji ni Cyllile Muhongya na Jaribu muliwavyo wote wakiwa Mashariki mwa DRC.

 • DRC ipo tayari kwa Uchaguzi wa Desemba 30, 2018 ?

  DRC ipo tayari kwa Uchaguzi wa Desemba 30, 2018 ?

  26/12/2018 Duração: 17h07min

  Wananchi wa DRC, wanatarajiwa kupiga kura siku ya Jumapili kumchagua rais mpya na viongozi wengine, baada ya zoezi hilo kuahirishwa kwa wiki moja baada ya kuteketea kwa jengo la kuhifadhi vifaa vya kupigia kura jijini Kinshasa. Tunajadili hili, tukiwa na Steven Chondo, mmoja wa maafisa wa kampeni wa mgombea wa chama tawala Emmanuel Shadary, lakini pia Reubens Mikindo , Naibu Katibu Mkuu wa chama kikuu cha upinzani UDPS, ambacho mgombea wake ni Felix Tshisekedi.

Informações: