Sinopse

Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.

Episódios

 • Siha Njema - Fistula Tishio kwa Wajawazito wanaochelewa kufika Hospitali wakati wa Uchungu

  Siha Njema - Fistula Tishio kwa Wajawazito wanaochelewa kufika Hospitali wakati wa Uchungu

  27/06/2019 Duração: 10min

  Kwa Mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) zaidi ya wasichana na wanawake milioni 4 ulimwenguni wanaishi na tatizo la Fistula huku wanawake kati ya  50,000 na 100,000 wakipata tatizo hili kila mwaka. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Siha Njema kuangazia Ugonjwa huo.

 • Lishe bora kwa watu wenye afya njema

  Lishe bora kwa watu wenye afya njema

  08/01/2019 Duração: 09h08min

  Makala ya siha njema juma hili inaangazia mlo bora kwa watu wasio na matatizo kiafya,ikiwa ni mwanzoni mwa mwaka jamii inashauriwa kuwa na maazimio ya kula vizuri pia...

 • Ripoti ya shirika la afya duniani yaonya kuhusu ongezeko la visa vya saratani

  Ripoti ya shirika la afya duniani yaonya kuhusu ongezeko la visa vya saratani

  18/09/2018 Duração: 10h06min

  Ripoti ya Shirika la afya duniani WHO kuhusu ongezeko la visa vipya vya saratani na vifo. Sabina Mpelo ameakuandalia makala hii kwa kuzungumza na watu mbalimbali akiwemo Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu

 • Maziwa ya mama ni kinga kwa afya ya mtoto

  Maziwa ya mama ni kinga kwa afya ya mtoto

  07/08/2018 Duração: 10min

  Leo makala ya siha njema inaangazia umuhimu wa unyonyeshaji maziwa ya mama baada ya kugundulika kuwa wanawake wengi hawatilii maanani suala hilo..

 • Fahamu kuhusu lishe bora kwa watoto

  Fahamu kuhusu lishe bora kwa watoto

  10/07/2018 Duração: 09min

  Karibu kuangazia umuhimu wa lishe bora kwa watoto,wataalamu wa afya kutoka jijini Dar es salaam wanaangazia maana ya lishe na kwa vipi jamii inaweza kuwapatia watoto ili kusaidia ukuaji mzuri..

 • Fistula inatibika jamii yatakiwa kuwasaidia waathirika

  Fistula inatibika jamii yatakiwa kuwasaidia waathirika

  26/06/2018 Duração: 08min

  Jamii imetakiwa kuwasaidia waathirika wa fistula badala ya kuwabagua na kuwanyanyasa.Tatizo la Fistula linatibika kwa nchini Tanzania matibabu hutolewa bure katika hospitali ya CCBRT jijini Dar es salaam..fuatilia zaidi makala haya.

 • Fahamu tatizo la Autism au usonji na namna ya kukabiliana nalo

  Fahamu tatizo la Autism au usonji na namna ya kukabiliana nalo

  15/06/2018 Duração: 09min

  Makala ya siha njema juma hili inaangazia usonji,kitaalamu Autism ambapo shuhuda Lucy Ruhasha mtanzania anasimulia namna alivyogundua tatizo hilo kwa mwanae wa kwanza na kukabiliana nalo...

 • Umuhimu wa wakunga katika kupunguza vifo vya wanawake wakati wa kujifungua na watoto wachanga

  Umuhimu wa wakunga katika kupunguza vifo vya wanawake wakati wa kujifungua na watoto wachanga

  08/05/2018 Duração: 09min

  Dunia yaadhimisha siku ya wakunga na kubainisha umuhimu wao katika kupambana na vifo vya wanawake wajawazito na watoto wachanga wakati wa kujifungua..

 • Siku ya kupambana na ugonjwa wa malaria duniani

  Siku ya kupambana na ugonjwa wa malaria duniani

  01/05/2018 Duração: 08min

  Malaria bado ni tishio katika mataifa yanayoendelea hasa katika bara la Afrika,tunaangazi augonjwa huu wakati huu dunia ikiadhimisha siku ya malaria ya kimataifa..

 • Jema Baruani,Mtanzania anayeshuhudia kupona saratani ya mitoki

  Jema Baruani,Mtanzania anayeshuhudia kupona saratani ya mitoki

  24/04/2018 Duração: 10min

  Makala ya siha njema inaangazia saratani ya mitoki baada ya kutembelewa na shuhuda aliyeugua na kutibiwa ugonjwa huo nchini Tanzania Jema Baruani ambaye anatoa hamasa kwa jamii kuwa na utamaduni wa kupima afya mara kwa mara ili kujua hali ya afya kabla ya kushambuliwa na magonjwa.Karibu

 • Fahamu kuhusu Homa ya Dengue

  Fahamu kuhusu Homa ya Dengue

  27/03/2018 Duração: 09h06min

  Karibu kujifunza kuhusu homa ya Dengue ambayo   dalili zake ni homa ya ghafla, kuumwa kichwa, maumivu ya viungo na uchovu ...kufahamu mengi zaidi tegea sikio..

 • Kifafa cha mimba kinachangia vifo vya wajawazito na watoto

  Kifafa cha mimba kinachangia vifo vya wajawazito na watoto

  31/10/2017 Duração: 10h05min

  Wataalamu wanaangazia vifo vya watoto wachanga na wajawazito vinacvyochangiwa na tatizo la kifafa cha mimba katika siku za hivi karibuni.Daktari Daniel Nkungu bingwa wa matatizo ya kina mama akiwa Dar es salaam anazungumzia tatizo hili....

 • Uganda yathibitisha virusi vya Murbag

  Uganda yathibitisha virusi vya Murbag

  24/10/2017 Duração: 09min

  Karibu katika makala ya Siha Njema leo tunaangazia virusi vya Murbag ambavyo vimethibitika kuwepo nchini Uganda.Watu wawili wameelezwa kufariki dunia wakati huu kadhaa wakitengwa na kufanyiwa uchunguzi wa kiafya..kujua zaidi fuatana nami ..

 • Ugonjwa wa saratani ya matiti unatibika

  Ugonjwa wa saratani ya matiti unatibika

  17/10/2017 Duração: 10min

  Katika makala ya Siha njema,wakati dunia inapohimiza uelewa kwa jamii kuhusu ugonjwa wa saratani mnamo mwezi oktoba.Jamii inapaswa kufahamu kuwa ugonjwa huu unatibika..

 • Afya ya akili mahali pa kazi

  Afya ya akili mahali pa kazi

  10/10/2017 Duração: 09min

  Umoja wa mataifa unaadhimisha siku ya afya ya akili chini ya kauli mbiu afya ya akili mahali pa kazi.Nini wajibu wa muajiri na muajiriwa kuhakikisha tatizo la afya ya akili haliwapati kazini?

 • Ugonjwa wa kipindupindu watishia afya za wakazi Mashariki mwa DRCongo

  Ugonjwa wa kipindupindu watishia afya za wakazi Mashariki mwa DRCongo

  03/10/2017 Duração: 10min

  Makala ya Siha njema inaangazia ugonjwa wa kipindupindu uliopiga nchini DRC hivi karibuni na kuathiri idadi kubwa ya wakazi.Waziri wa afya jimboni kivu kaskazini na daktari mtafiti wanaangazia namna jami hiyo inavyokabiliana na maradhi hayo.

 • Lishe duni yachangia ongezeko la vifo katika jamii

  Lishe duni yachangia ongezeko la vifo katika jamii

  19/09/2017 Duração: 09min

  Makala ya siha njema inaangazia kuhusu lishe bora na umuhimu wake katika jamii,hivi karibuni ripoti ya shirika la afya la kimataifa imebainisha kuwa mtu mmoja hufariki dunia katika watu watano kwa kukosa lishe bora.Daktari Lucas Mkeni wa Dar es salaam Tanzania analiangazia hili...

 • Fahamu Juu ya Chazo,Dalili na Tiba ya Mambukizi Katika Njia ya Mkojo (U.T.I)

  Fahamu Juu ya Chazo,Dalili na Tiba ya Mambukizi Katika Njia ya Mkojo (U.T.I)

  17/01/2017 Duração: 10min

  Neno U.T.I ambalo ni ni kifupisho cha Urinary Tract infections,ambayo kwa lugha yetu ni maambukizi ya njia ya mkojo si geni katika masikioni mwa wengi, Ni tatizo kubwa ambalo hivi karibuni limetajwa kusumbua zaidi watoto wa kike na wanawake haswa kwa wanafunzi wanaotumia vyoo vya jumuiya. Basi leo kwa mara nyingine kupitia Makala yetu ya Siha Njema tutazungumzia juu ya tatizo la maambukizi katika njia ya mkojo Urinary Tract Infection,tatizo ambalo hivi karibuni linawasumbua sana watoto na wanawake  

 • Fahamu Juu ya Chanzo na Tiba ya Tatizo la Moyo

  Fahamu Juu ya Chanzo na Tiba ya Tatizo la Moyo

  03/01/2017 Duração: 09min

  Takwimu mbali mbali zikiwemo za WHO zinaonesha kuwa watoto wengi hufariki kabla ya mwaka mmoja kwa ugonjwa wa moyo bila kugundulika na kupatiwa matibabu ya haraka. Na tunaelezwa kuwa matatizo ya kuzaliwa ya moyo hutokea katika watoto wanne hadi 9 katika kila vichanga 1,000 vinavyozaliwaBasi katika sehemu yetu ya Pili ya Makala ya siha Njema juma hili tunangazia juu ya tatizo la moyo kwa watoto

 • Fahamu Juu ya tatizo la Moyo Kwa Watoto

  01/01/2017 Duração: 09min

Informações: