Sinopse

Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa

Episódios

 • Wimbi la Siasa - Matukio makubwa tuliyoyapa uzito mwaka 2019

  Wimbi la Siasa - Matukio makubwa tuliyoyapa uzito mwaka 2019

  27/12/2019 Duração: 09min

  Haya ndio makala ya mwisho ya Wimbi la Siasa mwaka 2019, tunaangazia matukio makubwa tuliyoyapa uzito kisiasa barani Afrika na kwingineko duniani.

 • Wimbi la Siasa - Nini suluhu ya kisiasa kuhusu mzozo wa kuwavamia wageni nchini Afrika Kusini ?

  Wimbi la Siasa - Nini suluhu ya kisiasa kuhusu mzozo wa kuwavamia wageni nchini Afrika Kusini ?

  06/09/2019 Duração: 09min

  Je, kuna suluhu ya kisiasa kuhusu mzozo wa wageni kuvamiwa na maduka yao kuvunjwa  nchini Afrika Kusini ?Tunajadili hili katika Makala ya Wimbi la Siasa.

 • DRC yampata rais mpya, historia yaandikwa

  DRC yampata rais mpya, historia yaandikwa

  24/01/2019 Duração: 09min

  DRC imempata rais mpya, Felix Thisekedi. Nchi hiyo ya Afrika ya Kati imeshuhudia ubadilishanaji wa madaraka kwa njia ya amani kwa mara ya kwanza tangu ilipopata uhuru mwaka 1960. Tunajadili hili kwa kina.

 • Tume ya Uchaguzi yahairisha Uchaguzi katika baadhi ya maeneo, Mashariki mwa DRC

  Tume ya Uchaguzi yahairisha Uchaguzi katika baadhi ya maeneo, Mashariki mwa DRC

  27/12/2018 Duração: 09min

  Hatimaye, Uchaguzi Mkuu wa DRC utafanyika siku ya Jumapili, lakini Tume ya Uchaguzi imeahirisha zoezi hilo katika maeneo ya Butembo, Beni na Yumbi kwa sababu za kiusalama na maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola.

 • Uchaguzi Mkuu wa DRC wahairishwa

  Uchaguzi Mkuu wa DRC wahairishwa

  20/12/2018 Duração: 09min

  Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo uliokuwa umepangwa kufanyika tarehe 23 mwezi Desemba, sasa umeahirishwa hadi tarehe 30 baada ya kuteketea kwa ghala la kuhifadhi vifaa vya kupigia kura jijini Kinshasa.

 • Kampeni za DRC zakumbwa na vurugu

  Kampeni za DRC zakumbwa na vurugu

  13/12/2018 Duração: 09min

  Siku 10 kuelekea Uchaguzi Mkuu nchini DRC, mauaji yameripotiwa katika kampeni za siasa hasa katika mikutano ya Martin Fayulu, mgombea vya vyama upinzani lakini pia kuteketea moto kwa jengo la kuhifadhi vifaa vya kupigia kura jijini Kinshasa. Tunajadili hili kwa kina.

 • Rais Salva Kiir agoma kuunda mahakama maalum Sudan Kusini

  Rais Salva Kiir agoma kuunda mahakama maalum Sudan Kusini

  04/10/2018 Duração: 10h04min

  Serikali ya Sudan Kusini imetupilia mbali wito uliotolewa na Umoja wa Mataifa pamoja na Umoja wa Afrika wa kutaka serikali hiyo iunde mahakama maalum ya kushughulikia watuhumiwa wa makosa ya uhalifu wa kivita yaliyotekelezwa katika kipindi cha mapigano yaliyozuka mwaka 2013 ikiwa ni miaka miwili tangu nchi hiyo ipate uhuru kutoka Sudan. Je unajua kwa nini Serikali ya Sudan Kusini imegoma kutekeleza woto huo? Fuatilia Makala ya Wimbi Siasa na Victor Robert Wile kujua kulikoni?

 • Rais Salva Kiir atangaza kamati ya mpito

  Rais Salva Kiir atangaza kamati ya mpito

  27/09/2018 Duração: 09min

  Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ameteua tume ambayo itaratibu mchakato wa kuundwa kwa serikali ya mpito ambayo baadaye itakaa madarakani kwa miaka mitatu kabla ya kufanyika uchaguzi wa kidemokrasia, je hatua hiyo itakua mwarobaini wa kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe na kuleta amani ya kudumu? Ungana na Victor Robert Wile katika makala ya Wimbi la Siasa.

 • Tume Huru ya Uchaguzi DRC, CENI yatangaza majina ya wagombea Urais

  Tume Huru ya Uchaguzi DRC, CENI yatangaza majina ya wagombea Urais

  20/09/2018 Duração: 10h04min

  Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi CENI nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC, Corneille Nangaa ametangaza majina ya wagombea urais katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Disemba 23 mwaka huu huku wanasiasa wa upinzani Jean Pierre Bemba na mwenzake Moise Katumbi wakikosa nafasi ya kugombea kutokana na sababu mbalimbali. Je unataka kujua nguvu ya upinzani inasimama katika nafasi gani? Ungana na Victor Robert Wile katika Makala haya ya Wimbi la Siasa.

 • Mgogoro wa Sudan Kusini bado kitendawili hata bada ya kusainiwa kwa mkataba

  Mgogoro wa Sudan Kusini bado kitendawili hata bada ya kusainiwa kwa mkataba

  13/09/2018 Duração: 09min

  Hali ya Sudan Kusini bado ni tete hata baada ya kusainiwa kwa makataba wa amani wa mwisho wakati huu kukiendelea kushuhudiwa mapigano katika baadhi ya maeneo nchini humo. Je suala la kupatikana kwa amani nchini Sudan Kusini linakwamishwa vipi na nani wa kulaumiwa kama mkataba mpya amani hautatekelezwa? lakini nini mustakabali wa taifa hilo changa? Makala ya Wimbi la Siasa kupitia kwa Mtayarishaji na Mtangazaji wako Victor Robert Wile inakupa picha nzima kuhusiana na Sudan Kusini.

 • Jean Pierre Bemba hatihati kugombea Urais DRC

  Jean Pierre Bemba hatihati kugombea Urais DRC

  06/09/2018 Duração: 10h01min

  Majina ya wagombea Urais ya awali yametangazwa huku Jean Pierre Bemba akienguliwa na yeye kuapa kukata rufaa kugai haki yake wakati Tume huru ya Uchaguzi CENI ikidai hawezi kugombea kutokana na kesi yake katika mahakama ya ICC. Je unafikiri hali itakuaje na nini hatima ya kiongozi huyo wa upinzani? Ungana na Victor Robert Wile katika Makala ya Wimbi la Siasa kupata undani wa suala hilo.

 • Rais Joseph Kabila kubadilisha Katiba kuwania tena urais ?

  Rais Joseph Kabila kubadilisha Katiba kuwania tena urais ?

  31/05/2018 Duração: 10min

  Kuna dalili kuwa rais Joseph Kabila wa DRC anapanga kuibadilisha Katiba ili kuwania urais kwa muhula wa tatu. Mabango ya picha ya rais Kabila,  yaliyo na maandishi "Huyu ndio mgombea wetu" yameonekana jijini Kinshasa. Hii inamaanisha nini ? Tunajadili.

 • Tume ya Uchaguzi nchini DRC CENI yapata mitambo ya kuwatambua wapiga kura

  Tume ya Uchaguzi nchini DRC CENI yapata mitambo ya kuwatambua wapiga kura

  23/02/2018 Duração: 10h04min

  Tume ya Uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo CENI, imepata mitambo ya kieletroniki kuwatambua wapiga kura wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi Desemba. Je, mitambo hii itsaidia Uchaguzi huo kuwa huru na haki ? Tunajadili hili na mbunge wa Francois Rubota kutoka muungano unaomuunga mkono rais Joseph Kabila, Majorite Preidentielle, lakini pia Naibu Katibu Mkuu wa chama Kikuu cha upinzani UDPS Reubens Mikindo.

 • Kenya yaendelea kushuhudia mzozo wa kisiasa

  Kenya yaendelea kushuhudia mzozo wa kisiasa

  11/01/2018 Duração: 09min

  Kenya imeendelea kushuhudia mzozo wa kisiasa, baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka uliopita. Kiongozi wa upinzani NASA Raila Odinga, amekataa kumtambua rais Uhuru Kenyatta na amesema ataapishwa kama rais wa watu tarehe 30 mwezi Januari mwaka huu. Je, kuna nafasi ya mazungumzo katika mzozo huu.

 • Maandamano ya Nchi ya Iran na amna Mataifa ya Magharibi Yalivyo na Mkono

  Maandamano ya Nchi ya Iran na amna Mataifa ya Magharibi Yalivyo na Mkono

  04/01/2018 Duração: 09min

  Makala ya Wimbi la Siasa Juma Hili Inaangazia Hali ya Kisiasa Nchini Iran Ambayo Kwa Majuma Kadhaa Imeshuhudia Maandamano ya Wananchi Wakipinga Hali Ngumu ya Maisha. Hata Hivyo Juma Hili Pia Wafuasi Wanaoiunga Mkono Serikali Nao Walifanya Maandamano Kuonesha uungaji Mkono Wao Kwa Serikali. Nini Hatma ya Siasa ya Nchi ya Iran? Ni Kweli Nchi za Magharibi Zina Mkono na Vurugu Zilizoshuhudiwa Iran?

 • Matukio makubwa ya kisiasa mwaka 2017

  Matukio makubwa ya kisiasa mwaka 2017

  28/12/2017 Duração: 10min

  Mwaka 2017, ulikuwa na mwaka wa kisiasa hasa barani Afrika. Uchaguzi tata nchini Kenya, siasa za Uchaguzi nchini DRC, Gambia kumpata rais mpya, Robert Mugabe kujiuzulu baada ya kuongoza Zimbabwe tangu 1980 na wabunge nchini Uganda kubadilisha Katiba. Tunakukumbusha mambo yalivyokuwa.

 • Wabunge nchini wabadilisha Katiba

  Wabunge nchini wabadilisha Katiba

  21/12/2017 Duração: 10h06min

  Wabunge nchini Uganda, wamebadilisha Katiba ya nchi hiyo kwa kuondoa kikomo cha mtu anayetaka kuwania urais nchini humo kutoka miaka 75. Hii inampa nafasi rais Yoweri Museveni kuwania tena urais mwaka 2021, akiwa na miaka 76. Upinzani umesema utakwenda Mahakamani kupinga mabadiliko hayo.

 • Nkurunziza azindua kampeni ya kuibadilisha Katiba

  Nkurunziza azindua kampeni ya kuibadilisha Katiba

  14/12/2017 Duração: 10min

  Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, amezindua kampeni ya kuibadilisha Katiba ya nchi hiyo, lenye lengo la kuongeza muda wa rais kukaaa madarakani kutoka miaka mitano hadi miaka saba. Iwapo mabadiliko hayo yatapitishwa, Nkurunziza ana nafasi ya kuwania tena uongozi wa nchi hiyo mwaka 2020 na kuongoza mihula miwili hadi 2034. Hii ni mbinu ya Nkurunziza kuendelea kukaa madarakani ?

 • Majaji wa Mahakama ya Juu nchini Kenya kuamua hatima ya ushindi wa Kenyatta

  Majaji wa Mahakama ya Juu nchini Kenya kuamua hatima ya ushindi wa Kenyatta

  09/11/2017 Duração: 09min

  Mahakama ya Juu nchini Kenya inatarajiwa kuanza kusikiliza kesi za kupinga uchaguzi wa marudio uliofanyika Oktoba 26, 2017 ukidaiwa kuwa haukuwa huru, haki na wa kuaminika. Swali ni je majaji wa mahakama hiyo watafuta tena uchaguzi kama ilivyokua katika uchaguzi wa Agosti 8 mwaka huu ? Makinika na Victor Robert Wile katika Makala ya Wimbi la Siasa kupata uchambuzi wa kina.

 • Ziara ya Rais Salva Kiir nchini Sudani na changamoto za mgogoro wa kisiasa

  Ziara ya Rais Salva Kiir nchini Sudani na changamoto za mgogoro wa kisiasa

  02/11/2017 Duração: 10h02min

  Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir hivi karibuni alifanya ziara nchini Sudan Kharthoum na kufanya mazungumzo na Rais wa nchi hiyo Omar Al Bashir wakilenga kuimarisha uhusiano na kuondoa hali ya wasiwasi baina ya pande hizo mbili kutokana na kushutumiana mara kwa mara kila upande ukilaumu upande mwingine kwa kusaidia waasi. Ziara hiyo inaweza kuwa mwarobaini wa mgogoro wa Sudani Kusini? Ungana na Victor Robert Wile katika Makala haya ya Wimbi la Siasa kujua mustakabali wa Sudani Kusini.

Informações: