Sinopse

Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.

Episódios

 • Jua Haki Zako - Tamko la Afrika kuhusu demokrasia chaguzi huru na utawala bora linatekelezeka?

  Jua Haki Zako - Tamko la Afrika kuhusu demokrasia chaguzi huru na utawala bora linatekelezeka?

  04/02/2020 Duração: 10min

  Imetimia miaka 13 tangu bara la Afrika kuridhia tamko la demokrasia, utawala bora na chaguzi huru za haki. Tunaangazia tamko hilo na wajibu wa viongozi na asasi za kiraia kukuza demokrasia barani Afrika. Ungana na Fredrick Nwaka katika makala ya Jua haki zako akizungumza na Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC, Ana Henga

 • Jua Haki Zako - Fahamu kuhusu utaratibu wa kisheria baada ya kuvunjika kwa uchumba

  Jua Haki Zako - Fahamu kuhusu utaratibu wa kisheria baada ya kuvunjika kwa uchumba

  02/12/2019 Duração: 09min

  Mara kadhaa katika mataifa ya Afrika kumeripotiwa matukio ya kuvunjika kwa uchumba baina ya mwanaume na mwanamke waliokuwa na matarajio ya kufunga ndoa. Je utaratibu wa kisheria ukoje? Ungana na Fredrick Nwaka katika makala ya Jua Haki Zako

 • Jua Haki Zako - Ulimwengu waadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake huku vitendo hivyo badoi vikiripotiwa katika mataifa mbalimbali

  Jua Haki Zako - Ulimwengu waadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake huku vitendo hivyo badoi vikiripotiwa katika mataifa mbalimbali

  26/11/2019 Duração: 09min

  Dunia inaadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na wasichana huku kundi hili likikabiliwa na changamoto mbal;imbali kama ndoa za utotoni, kudhalilishwa na kupigwa, ukatili wa kingono n.k. Ungana na Fredrick Nwaka aliyekuandalia makala ya Jua Haki Zako.

 • Jua Haki Zako - Haki ya mwajiri na mwajiriwa kwa kuzingatia misingi ya mikataba ya kimataifa na kikanda

  Jua Haki Zako - Haki ya mwajiri na mwajiriwa kwa kuzingatia misingi ya mikataba ya kimataifa na kikanda

  18/11/2019 Duração: 10min

  Makala ya Jua haki zako wiki hii inaangazia haki za mwajiri na mwajiriwa kulingana na mikataba ya kimataifa, kikanda na sheria za nchi mbalimbali. Ungana na Fredrick Nwaka akizungumza na mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Tanzania Tito Magoti hasa wakiangazia ripoti ya haki za binadamu na biashara iliyotolewa na kituo cha sheria na haki za binadamu ya mwaka 2018/19.

 • Jua Haki Zako - Ukatili wa kijinsia na wajibu wa raia na serikali kukabiliana na vitendo hivyo

  Jua Haki Zako - Ukatili wa kijinsia na wajibu wa raia na serikali kukabiliana na vitendo hivyo

  12/08/2019 Duração: 09min

  Matukio ya ukatili wa kijinsia bado ni changamoto katika mataifa ya Afrika mashariki na kati, tunaangazia namna utafiti na sheria zinavyoweza kusaidia kutatua changamoto hii. Ungana na Fredrick Nwaka aliyekuandalia makala haya

 • Jua Haki Zako - Umoja wa Mataifa unatekeleza kwa vitendo ulinzi wa haki za binadamu

  Jua Haki Zako - Umoja wa Mataifa unatekeleza kwa vitendo ulinzi wa haki za binadamu

  16/06/2019 Duração: 10min

  Makala ya Jua Haki Zako juma hili inaangazia ikiwa umoja wa Mataifa unatekeleza kwa vitendo kuhusu ulinzi wa haki za binadamu kiduni.

 • Jua Haki Zako - Ripoti ya shirika la save the children kuhusu hali ya watoto

  Jua Haki Zako - Ripoti ya shirika la save the children kuhusu hali ya watoto

  16/06/2019 Duração: 10min

  Makala ya Jua Haki Zako juma hili inaitazama kwa kina ripoti ya shirika la kimataifa la Save the Children iliyoangazia hali ya watoto duniani.

 • Jua Haki Zako - Uwepo wa vituo vya Mateso kwenye mataifa

  Jua Haki Zako - Uwepo wa vituo vya Mateso kwenye mataifa

  16/06/2019 Duração: 10min

  Makala ya Jua Haki Zako juma hili inajadili kuhusu uwepo wa vituo vya kutesea ambavyo vimetengenezwa kwa siri na serikali mbalimbali duniani kwa lengo la kuwahoji kwa njia ya mateso watuhumiwa ili kupata ukweli.

 • Jua Haki Zako - Ripoti ya LHRC kuhusu ukatili wa kingono dhidi ya watoto nchini Tanzania

  Jua Haki Zako - Ripoti ya LHRC kuhusu ukatili wa kingono dhidi ya watoto nchini Tanzania

  16/06/2019 Duração: 10min

  Makala ya Jua Haki Zako juma hili inaidadavua kwa kina ripoti ya kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania LHRC kuhusu ukatili wa kingono dhidi ya watoto.

 • Jua Haki Zako - Haki za Wanawake na Watoto Nchini Tanzania

  Jua Haki Zako - Haki za Wanawake na Watoto Nchini Tanzania

  16/06/2019 Duração: 10min

  Makala ya Jua Haki Zako juma hili inazungumza na wanaharakati wa nchini Tanzania ambao wanafanya sanaa ya muziki na wanatumia muziki kufikisha ujumbe kuhusu kuheshimiwa kwa haki za watoto nchini Tanzania. Sikiliza makala ya juma hili.

 • Jua Haki Zako - Dhana ya utawala bora barani Afrika na haki za binadamu

  Jua Haki Zako - Dhana ya utawala bora barani Afrika na haki za binadamu

  16/06/2019 Duração: 09min

  Makala ya Jua Haki Zako juma hili inajadili kwa kina kuhusu dhana ya utawala bora barani Afrika, kwanini viongozi wengi wa Afrika wanangangania kukaa madarakani hata baada ya muhula wao? Kwanini wanashuhudia utekelezaji wa vitendo vya unyanyasaji na ukatili dhidi ya raia wao? fuatilia makala haya.

 • Jua Haki Zako - Ripoti ya Amnesty International kuhusu utekelezwaji wa adhabu ya kifo duniani

  Jua Haki Zako - Ripoti ya Amnesty International kuhusu utekelezwaji wa adhabu ya kifo duniani

  16/06/2019 Duração: 09min

  Makala ya Jua Haki Zako juma hili inaangazia ripoti ya shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International kuhusu utekelezaji wa adhabu ya kunyonga duniani, unajua ni mataifa mangapi bado yananyonga na yale ambayo yameacha kunyonga? Fuatilia makala haya.

 • Jua Haki Zako - Dunia inajifunza nini kutokana na mauaji ya kimbari na kuheshimu haki za binadamu

  Jua Haki Zako - Dunia inajifunza nini kutokana na mauaji ya kimbari na kuheshimu haki za binadamu

  16/06/2019 Duração: 10min

  Makala ya Jua Haki Zako juma hili inaangazia maadhimisho ya mauaji ya kimbari, ikitazama kwa kina ni ikiwa dunia imejifunza kutokana na ukatili na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliotekelezwa wakati wa mauaji ya Kimbari.

 • Jua Haki Zako - Haki za Watoto: Dhulma za Kingono pwani ya Kenya

  Jua Haki Zako - Haki za Watoto: Dhulma za Kingono pwani ya Kenya

  16/06/2019 Duração: 10min

  Makala ya Jua Haki Zako juma hili inaangazia ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto pwani ya Kenya. Karibu usikilize makala haya.

 • Jua Haki Zako - Sheria za makosa ya ubakaji Afrika Mashariki

  Jua Haki Zako - Sheria za makosa ya ubakaji Afrika Mashariki

  16/06/2019 Duração: 10min

  Makala ya Jua Haki Zako juma hili inaangazia sheria za makosa ya ubakaji kwenye nchi za Afrika Mashariki, je zinafanya kazi vema kuzuia ubakaji dhidi ya wasichana? Ungana na mtayarishaji wa makala haya.

 • Jua Haki Zako - Mpango wa kufunga kambi ya Daadab: Zipi haki za wakimbizi wanaoishi kwenye kambi

  Jua Haki Zako - Mpango wa kufunga kambi ya Daadab: Zipi haki za wakimbizi wanaoishi kwenye kambi

  16/06/2019 Duração: 10min

  Makala ya Jua Haki Zako juma hili inaangazia mpango wa Serikali ya Kenya kutaka kuifunga kambi kubwa ya wakimbizi duniani ya Daadab, je hatua hii watetezi wa haki za binadamu wanaitazamaje? Makala ya juma hili inatathmini hatua ya Kenya kwa kina.

 • Haki ya Kupata Dhamana kwa Mtuhumiwa Sehemu ya Pili

  Haki ya Kupata Dhamana kwa Mtuhumiwa Sehemu ya Pili

  11/03/2019 Duração: 10h04min

  Karibu katika Sehemu ya pili Katika Makala Haya tukiangazia Haki ya kupata Dhamana kwa Mtuhumiwa. Unagana na Steven Mumbi katika Makala haya akizungumza na Wakili wa Kujitegemea kutoka nchini Tanzania, Jebra Kambole katika sehemu ya pili ya Haki ya Kupata Dhamana, karibu Msikilizaji.

 • Haki ya Kupata Dhamana kwa Mtuhumiwa

  Haki ya Kupata Dhamana kwa Mtuhumiwa

  04/03/2019 Duração: 06min

  Katika Makala Haya tunaangazia Haki ya kupata Dhamana kwa Mtuhumiwa. Unagana na Steven Mumbi katika Makala haya akizungumza na Wakili wa Kujitegemea kutoka nchini Tanzania, Jebra Kambole katika sehemu ya kwanza ya Haki ya Kupata Dhamana, karibu Msikilizaji.

 • Kuzimwa kwa Internet DRC ni ukiukaji wa haki za binadamu?

  Kuzimwa kwa Internet DRC ni ukiukaji wa haki za binadamu?

  07/01/2019 Duração: 09min

  Makala ya Jua Haki Zako juma hili inaangazia hatua ya kuzimwa kwa huduma ya mtandao {Internet} nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, je kitendo kilichofanywa na Serikali kinakiuka haki za binadamu? Ungana na mtayarishaji wa makala haya pamoja na wakili Ojwan'g Agina.

 • Tathimini ya haki za binadamu barani Afrika mwaka 2018 na matarajio ya 2019

  Tathimini ya haki za binadamu barani Afrika mwaka 2018 na matarajio ya 2019

  24/12/2018 Duração: 09min

  Bara la Afrika mwaka 2018 limekabiliwa na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu ikiwemo mauaji, utekaji nyara, utungwaji wa sheria zinazokinzana na uhuru wa kujieleza na kukusanyika. Fredrick Nwaka amekuandalia makala haya ya Jua haki zako.

Informações: