Sinopse

Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.

Episódios

 • Habari RFI-Ki - Rwanda na Uganda zabadilishana wafungwa zikilenga kutafuta suluhu ya mzozo wa kidiplomasia baina yao

  Habari RFI-Ki - Rwanda na Uganda zabadilishana wafungwa zikilenga kutafuta suluhu ya mzozo wa kidiplomasia baina yao

  04/02/2020 Duração: 09min

  Nchi za Rwanda na Uganda zimekubaliana kubadilishana wafungwa huku viongozi wa mataifa hayo wakitarajia kukutana katika mpaka wa Gatuna, ikiwa na hatua ya karibuni zaidi ya kutafuta suluhu ya mzozo wa kidiplomasia baina ya mataifa hayo. Fredrick Nwaka amekuandalia makala haya kwa kuzungumza na wasikilizaji wetu.

 • Habari RFI-Ki - Hatua ya Uganda kuachilia wanyarwanda tisa inaweza kupunguza joto la uhasama baina ya mataifa hayo mawili?

  Habari RFI-Ki - Hatua ya Uganda kuachilia wanyarwanda tisa inaweza kupunguza joto la uhasama baina ya mataifa hayo mawili?

  10/01/2020 Duração: 09min

  Serikali ya Uganda imetangaza kuwaachilia huru raia tisa wa Rwanda waliokuwa wakishikiliwa katika kambi za kijeshi nchini humo. Je hatua hii inaweza kupunguza joto la mvutano uliopo baina ya Kampala na Kigali. Ungana na Fredrick Nwaka aliyekuandalia makala haya kwa kuzungumza na wasikilizaji.

 • Habari RFI-Ki - Ni tukio gani unalikumbuka kwa mwaka 2019

  Habari RFI-Ki - Ni tukio gani unalikumbuka kwa mwaka 2019

  01/01/2020 Duração: 10min

  Mwaka 2019 unafikia ukingoni leo Disemba 31 na tunakupa fursa msikilizaji kutoa maoni yako kuhusu matukio muhimu yaliyotokea katika jamii yako. Ungana na Fredrick Nwaka aliyekuandalia makala haya.

 • Habari RFI-Ki - Umoja wa Mataifa washutumu serikali ya Sudani Kusini kwa kuajiri wapiganaji katika vyombo vya usalama na ujasusi

  Habari RFI-Ki - Umoja wa Mataifa washutumu serikali ya Sudani Kusini kwa kuajiri wapiganaji katika vyombo vya usalama na ujasusi

  30/11/2019 Duração: 10min

  Umoja wa mataifa umelaani vikali hatua ya serikali ya rais Salva Kiir kuajiri wapiganaji katika vyombo vya usalama huku pia ukinyooshea kidole Kenya na Uganda kwa kushindwa kusaidia mchakato wa amani nchini Sudani Kusini. Fredrick Nwaka amezungumza na wasikilizaji ili kupata maoni yao.

 • Habari RFI-Ki - Jumuiya ya Afrika Mashariki yatimiza miaka 20 tangu ilipoasisiwa kwa mara ya pili

  Habari RFI-Ki - Jumuiya ya Afrika Mashariki yatimiza miaka 20 tangu ilipoasisiwa kwa mara ya pili

  30/11/2019 Duração: 10min

  Jumuiya ya Afrika mashariki imetimiza miaka 20 tangu ilipoasisiwa kwa mara ya pili mwaka 1999. Fredrick Nwaka amekuandalia makala haya kwa kuzungumza  na wasikilizaji ikiwa jumuiya hiyo imetimiza malengo yake au imesalia kuwa jumuiya ya viongozi.

 • Habari RFI-Ki - Watu wenye ulemavu wa ngozi katika mataifa jirani na Tanzania bado wanakabiliwa na hatari ikiwemo mauaji

  Habari RFI-Ki - Watu wenye ulemavu wa ngozi katika mataifa jirani na Tanzania bado wanakabiliwa na hatari ikiwemo mauaji

  24/11/2019 Duração: 10min

  Shirika la Under The Same Sun lenye makao yake makuu nchini Canada linasema Tanzania imepiga hatua katika kukabiliana na madhila yanayowapata watu wenye ulemavu wa ngozi huku likisema mataifa jirani na Tanzania bado watu wenye ulemavu wa ngozi wanakabiliwa visa ikiwemo mauaji. Fredrick Nwaka ameandaa makala haya kwa kuzungumza na wasikilizaji. Ungana naye.

 • Habari RFI-Ki - Ufaransa na Umoja wa Ulaya utaweza kukomesha mauaji mashariki mwa DRC?

  Habari RFI-Ki - Ufaransa na Umoja wa Ulaya utaweza kukomesha mauaji mashariki mwa DRC?

  22/11/2019 Duração: 09min

  Daktari Dennis Mukwege ametoa wito kwa Ufaransa na umoja wa Ulaya kuingilia kijeshi nchini DRC ili kupambana na magaidi wa ADF wanaoendesha mauajio ya raia wilayani Beni na mashariki mwa nchi hiyo. Fredrick Nwaka amezungumza na wasikilizaji wetu ili kupata maoni yao.

 • Habari RFI-Ki - Rais Paul Kagame aonya nchi yoyote itakayochezea amani na usalama wa taifa lake

  Habari RFI-Ki - Rais Paul Kagame aonya nchi yoyote itakayochezea amani na usalama wa taifa lake

  17/11/2019 Duração: 10min

  Rais Paul Kagame wa Rwanda ametoa onyo kali kwa taifa lolote litakalochezea amani na usalam wa Rwanda, onyo linalokuja baada ya kuahirishwa kwa mazungumza baina ya Kigali na Kampala yanayolenga kumaliza mvutano uliopo baina ya mataifa hayo mawili. Fredrick Nwaka amekuandalia makala haya kwa kuzungumza na wasikilizaji.

 • Habari RFI-Ki - Ulimwengu waadhimisha siku ya kisukari huku idadi ya watu wanaougua maradhi hayo ikiongezeka

  Habari RFI-Ki - Ulimwengu waadhimisha siku ya kisukari huku idadi ya watu wanaougua maradhi hayo ikiongezeka

  17/11/2019 Duração: 10min

  Ulimwengu unaadhimisha siku ya kisukari duniani huku idadi ya watu wanaougua maradhi hayo ikiongezeka kutoka milioni 108 mwaka 1980 hadi milioni 420 mwaka 2014. Mtindo wa maisha unatajwa kuwa mojawapo ya sababu. Je kubadili mtindo wa maisha kunaweza kusaidia kukabiliana na maradhi haya? Ungana na Fredrick Nwaka aliyekuandalia makala haya kwa kuzungumza na wasikilizaji.

 • Habari RFI-Ki - Umoja wa Mataifa wasema kuna hali ya hofu nchini Burundi

  Habari RFI-Ki - Umoja wa Mataifa wasema kuna hali ya hofu nchini Burundi

  06/09/2019 Duração: 10min

  Tume ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Burundi imebaini katika ripoti yake kwamba "hali ya hofu" inatawala katika nchi hiyo, ikiwa imesalia miezi minane kabla ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2020. Katika ripoti yake, Tume ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Burundi, iliyoundwa na Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 2016, inaelezea jinsi mamlaka nchini humo na vijana wa chama tawala, Imbonerakure, wanaendelea kuwafanyia vitisho raia kwa kuwalazimisha kujiunga, kuunga mkono au kuchangia chama tawala, CNDD-FDD. Fredrick Nwaka amekuandalia makala haya kwa kuzungumza na wasikilizaji wetu

 • Habari RFI-Ki - Wiki ya unyonyeshaji yaadhimishwa duniani kote

  Habari RFI-Ki - Wiki ya unyonyeshaji yaadhimishwa duniani kote

  07/08/2019 Duração: 09min

  Dunia inaadhimisha wiki ya unyonyeshaji huku shirika la umoja wa mataifa la watoto UNICEF likitoa wito kwa familia, jamii na serikali duniani kote kuandaa mazingira wezeshi kwa akina mama kunyonyesha watoto katika mazingira ya kazi. Fredrick Nwaka amekuandalia makala haya kwa kuzungumza na wasikilizaji wetu

 • Habari RFI-Ki - Nini kifanyike ili kuzuia biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu?

  Habari RFI-Ki - Nini kifanyike ili kuzuia biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu?

  30/07/2019 Duração: 10min

  Siku ya kimataifa ya kupinga biashara haramu usafirishaji wa binadamu ambayo huadhimishwa duniani kote ifikapo julai 3o kila mwaka. Fredrick Nwaka amekuandalia makala haya kwa kuzungumza na wasikilizaji wetu ili kupata maoni yao.

 • Habari RFI-Ki - Kauli ya Donald Trump ilivyoleta hisia tofauti duniani

  Habari RFI-Ki - Kauli ya Donald Trump ilivyoleta hisia tofauti duniani

  17/07/2019 Duração: 10min

  Donald Trump, rais wa Marekani ametoa kauli kali ya kuwataka wabunge wanne wa Democrats kurudi waliokotoka, matamshi ambayo yamezua hofu huku wabunge hao wakimshutumu Trump kwa matamshi ya ubaguzi na kumtaka aombe radhi. Fredrick Nwaka amekuandalia makala haya kwa kuzungumza na wasikilizaji ili kupata maoni yao

 • Habari RFI-Ki - Jean-Pierre Bemba areje DRC kwa Kishindo

  Habari RFI-Ki - Jean-Pierre Bemba areje DRC kwa Kishindo

  27/06/2019 Duração: 10min

  Ungana na Steven Mumbi katika Makala haya akizungumza na Wasikilizaji wa Rfi Kiswahili kuhusu kurejea DRC Kwa Makamu wa zamani wa Rais wa nchi hiyo Jean-Pierre Bemba.

 • Habari RFI-Ki - Nchi za Afrika mashariki zinachukua tahadhari baada ya mlipuko wa ebola nchini Uganda

  Habari RFI-Ki - Nchi za Afrika mashariki zinachukua tahadhari baada ya mlipuko wa ebola nchini Uganda

  13/06/2019 Duração: 10min

  Ugonjwa wa ebola umeripotiwa kuingia nchini Uganda katika wilaya ya Kasese, Je mataifa ya Afrika mashariki yanachukua hatua zipi? Fredrick Nwaka amekuandalia makala ya habari rafiki kwa kuzungumza na wasikilizaji wetu

 • Habari RFI-Ki - Kampeni ya waandamanaji kutotii sheria nchini Sudan italazimisha jeshi kukabidhi mamlaka kwa raia?

  Habari RFI-Ki - Kampeni ya waandamanaji kutotii sheria nchini Sudan italazimisha jeshi kukabidhi mamlaka kwa raia?

  10/06/2019 Duração: 09min

  Waandamanaji nchini Sudan wameingia siku ya pili ya maandamano ya kutotii sheria ili kushinikiza jeshi kukabidhi madaraka kwa raia. Je hatua hiyo itafanikiwa? Ungana na Fredrick Nwaka aliyekuandalia makala haya kwa kuzungumza na wasikilizaji wetu.

 • Habari RFI-Ki - Moise Katumbi atafanikiwa kuviunganisha vyama vya upinzani nchini DRC?

  Habari RFI-Ki - Moise Katumbi atafanikiwa kuviunganisha vyama vya upinzani nchini DRC?

  27/05/2019 Duração: 10min

  Mwanasiasa wa upinzani nchini DRC, Moise Katumbi ametangaza kufanya ziara katika majimbo yote nchini humo kwa kile anasema ni kuunganisha vyama vya upinzani. Je atafanikiwa? Fredrick Nwaka amekuandalia makala haya kwa kuzungumza na wasikilizaji wetu

 • Habari RFI-Ki - Siku ya kimataifa ya wafanyakazi yaadhimishwa duniani kote

  Habari RFI-Ki - Siku ya kimataifa ya wafanyakazi yaadhimishwa duniani kote

  01/05/2019 Duração: 10min

  Ulimwengu leo unaadhimisha siku ya wafanyakazi huku wafanyakazi wakikabiliwa na changamoto mbalimbali. Je serikali za Afrika zinatia juhudi katika kutafuta majawabu ya changamoto zinazowakabili wafanyakazi. Fredrick Nwaka amekuandalia makala haya kwa kuzungumza na wasikilizaji wetu.

 • Habari RFI-Ki - Dunia ikiadhimisha siku ya wanawake, kundi hilo lina mchango katika kuibadilisha jamii?

  Habari RFI-Ki - Dunia ikiadhimisha siku ya wanawake, kundi hilo lina mchango katika kuibadilisha jamii?

  09/03/2019 Duração: 10min

  Machi 8 kila mwaka ulimwngu unaadhimisha siku ya wanawake. Je kuna mchango wa kundi hili katika kuibadili jamii? Fredrick Nwaka amezungumza na wasikilizaji wetu ili kupata maoni yao.

 • Habari RFI-Ki - Mzozo baina ya Rwanda na Uganda waathiri shughuli za kiuchumi

  Habari RFI-Ki - Mzozo baina ya Rwanda na Uganda waathiri shughuli za kiuchumi

  02/03/2019 Duração: 09min

  Mgogoro wa kidilpomasia baina ya Rwanda na Uganda umechukua sura mpya baada ya wafanyabiashara na wananchi wa Uganda kulalama kuzuiwa na maofisa wa Uganda kutumia mpaka wa Gatuna kwa shughuli za usafirishaji. Fredrick Nwaka amezungumza na wasikilizaji ili kupata maoni yao

Informações: